Local Bulletins

Kituo cha kuvutia watalii cha Illeret Footprint chazinduliwa rasmi.

Wito umetolewa kwa wakaazi wa Marsabit kutembelea vituo mbalimbali vya watalii hapa jimboni ili kuimarisha uchumi wa jimbo.

Kwa mujibu wa waziri wa jinsia na utalii katika kaunti ya Marsabit, Jeremiah Lendanyi, ni kuwa kaunti ya Marsabit ina vivutio vingi vya watalii na ambavyo vinaweza kuimarisha uchumi wa jimbo hili, ila lazima pia wenyeji wa Marsabit wavikumbatie.

Akizungumza na meza ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee siku moja baada ya kuzindua kituo cha kuvutia watalii kunachoonyesha nyayo za binadamu wa awali wa miaka milioni 1.5 iliyopita katika eneo la Illeret maarufu Illeret Footprint waziri Lendanyi amepongeza hatua ya kutunza na kuhifadhi maeneo muhimu kama hayo ambayo yawaweza kusaidia kuimarisha uchumi na biashara katika kaunti ya Marsabit.

Aidha waziri Lendanyi ametaja kwamba idara yake imejitolea kuhakikisha kwamba vivutio vya watalii hapa jimboni vinatunzwa na kuboreshwa kwa manufaa ya jamii.

Subscribe to eNewsletter