Gavana wa Marsabit Mohamud Ali apongeza rais Ruto kwa kuondoa hitaji la kupigwa msasa wakati wa kusaka kitambulisho….
February 6, 2025
NA CAROL WAFORO
Amri ya Rais William Ruto ya kuondoa hitaji la ukaguzi wakati wa kupata kitambulisho na stakabadhi nyingine kwa wakaazi wa eneo la kaskazini mwa kenya limeendelea kupongezwa na viongoni mbalimbali.
Akizungumza hii le katika kaunti ya Garissa wakati wa ziara ya rais Ruto kaskazini mashariki, gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali amedokeza kuwa vijana wanaoishi katika kaunti za wafugaji wamekumbwa na changamoto kupata kitambulisho cha taifa kwa muda sasa.
Gavana Ali amesema kuwa hatua hiyo itachangia pakubwa katika kusawazisha wakenya wote.
Aidha Gavana Ali pia amemuhahikishia rais William ruto ungwaji mkono kutoka kwa kaunti za wafugaji huku akionekana kumrushia vijembe aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kwa kugawanya taifa.
Hapo jana Rais William Ruto asaini amri ya kuwaondolea wakazi wa kaskazini mwa nchi hitaji la ukaguzi wakati wa kupata kitambulisho cha taifa
Huku akitoa agizo hilo, Rais William Ruto alisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa utawala wake kutekeleza umoja wa kitaifa na maendeleo katika maeneo yaliyotengwa.