Local Bulletins

ZAIDI YA ASILIMIA 60 YA MASHAMBA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAMEANDALIWA KWA AJILI YA ZOEZI LA UPANZI.

Zaidi ya asilimia 60 ya mashamba katika kaunti ya Marsabit yameandaliwa kwa ajili ya zoezi la upanzi.

Kwa mujibu wa afisa wa kilimo katika kaunti ya Marsabit Dub Nura ni kuwa zoezi hilo limeafanikishwa na ushirikiano kati ya idara ya kilimo jimboni Marsabit na mashirika mengine yasiyokuwa yakiserekali hapa jimboni.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Dub ametaja hoja ya wakulima kuandaa mashamba yao kutokana na mvua fupi inayotarajiwa kati ya mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu.

Aidha Dub Nura amewataka wakulima ambao wanauwezo wa kununua mbegu kufanya vile kwani serekali itao mbegu kwa wale wasiojiweza pekee.

Hata hivyo Dub Nura ameweka wazi kuwa idara ya kilimo kaunti ya Marsabit inaendeleza zoezi la mafunzo kwa wakulima ili kuhakikisha kwamba wanapata maarifa ya kuendeleza kilimo biashara.

Kwa upande wake chifu wa eneo la Songa Ali Dera Ibrahim ametaja kwamba kwa sasa wakulima wa eneo hilo wamejiandaa kikamilifu licha ya upungufu wa mbengu za kupanda.

Subscribe to eNewsletter