KITUO CHA KUOKOA WANAOPITIA DHULMA ZA KIJINSIA KUANZISHWA LOGLOGO KAUNTI YA MARSABIT
November 6, 2024
Wazazi Marsabit watakiwa kuwapa watoto wao ulinzi msimu huu wa likizo
Ni jukumu la Wazazi kuhakikisha kuwa usalama wa wanao umeisharishwa wakati huu wa likizo. Hayo ni kwa mujibu wa katibu wa muungano wa Maimamu katika kaunti ya Marsabit Sheikh Bashir Somo.
Akizungumza na idhaa hii, Sheikh Bashir amesema kuwa asilimia kubwa ya Watoto hupitia dhulma za kinjisia kutoka kwa watu wanaowajua akilaumu kitendo cha kumuacha mtoto nyumbani bila kujali atabakia na nani suala ambalo amelikashifu na kudai kuwa ndio huchangia katika dhulma za mapenzi kwa Watoto.
Sheikh Bashir ameelezea kuwa ni sharti mzazi awe karibu na mtoto ili aweze kujua changamoto anazopitia na pia kumshauri ipasavyo na kumsaidia katika kufanya maamuzi dhabiti katka maisha.
Kadhalika Kiongozi huyu ameitaka serekali kuweza kushirikiana na wazazi ili kupunguza visa vya Watoto kurandaranda mitaani na pia kusaida katika kutoa mafunzo kwa Watoto msimu huu wa likizo.
Kuhusiana na suala la wizi wa mtihani, sheikh Bashir ameilaani tendo hilo na kuitaja kama linalorejesha maendeleo ya elimu nyuma nchini.