Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Mwanaume wawili wenye umri wa makamu wamefikishwa katika mahakama ya Marsabit hii leo kwa kosa la wizi wa kimabavu.
Washukiwa Boru Wako Dida almarufu Boru Abakula na Abdirahaman Hussein almarufu Churuka wanadaiwa kuwa mnamo tarehe 3 mwezi wa septemba katika mtaa wa Saku wakiwa na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama wakiwa wamejihami na kifaa hatari walifanikiwa kumwiba Adan Gabre Yayo pikipiki inayogharimu shilingi 116,000.
Washukiwa walifikishwa mbele ya hakimu mkaazi Simon Arome na kukana mashtaka dhidi yao huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa tena tarehe 3 mwezi ujao