WAKAAZI WA MARSABIT WAONESHA MATUMAINI YA KESI ZAO KUKAMILISHWA HARAKA NA MFUMO WA AJS
November 22, 2024
Watu wanaoishi na ulemavu wa kutosikia na kuona katika kaunti ya Marsabit wamelalamikia kutengwa wakati wa zoezi la kusajili watu wanaoishi na ulemavu majuma machache yaliyopita
Kwa mujibu wa Asili Sori ambaye aliongea nasi kwa lugha ya ishara na kutafsiriwa kwa sauti na Bi Arbe ni kuwa watu wanaoishi na ulemavu wa kutosikia hawakusajiliwa kutokana kukosekana kwa mashine ambayo ilikuwa inasaidia kutambua iwapo wanaulemavu wa kutoona.
Sori ameitaka serekali kuu na serekali ya kaunti kuingilia kati na kununua mashine ambayo itarahisisha zoezi hilo.
Aidha Sori amesema kuwa watu wanaoishi na ulemavu wa kutoona na kusikia huwa wanakosa huduma kutoka kwa afisi za serekali kwa sababu ya kukosekana kwa mkalimani ambaye atawasaidia katika kutafsiri.
Kwa upande wake Stephen Dokhle ambaye pia ni mmoja wa watu watu wanaoishi na ulemavu amepongeza swala la kuwapa msaada wa kupata elimu akisema kuwa hilo limesaidia pakubwa kuhakikisha kwamba watoto wanaoishi na ulemavu wanapata elimu.
Aidha amesifia kile amekitaja kwamba ni misaada ya vifaa kutoka kwa baraza la watu wanaoishi na ulemavu huku akitaka baraza kuzidisha misaada hiyo.
Wakati uo huo, afisa wa idara ya huduma za jamii jimboni Marsabit, Habiba Ailo amewarai watu wanaoishi na ulemavu jimboni Marsabit kujitokeza ili waweze kuhusishwa katika masuala mbalimbali ya jamii.
Baraza la watu wanaoishi na ulemavu hii leo limeadhimisha miaka 20 tangu kuadhimishwa kwake huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni watu wanaoishi na ulemavu kuhusishwa katika miradi ya maendeleo, masomo, afya na mipangilio mbali mbali katika jamii.