Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Ni afueni kwa watu wanaoishi na Ulemavu katika kaunti ya Marsabit baada ya senEta wa kaunti hii Mohamed Chute akishirikiana na mbunge wa Sakuu Ali Raso kuwapa vifaa vya kuwasaidia.
Kwa mujibu wa mshirikishi katika ofisi mbunge wa Saku Bonaya Doti ni kuwa walemavu wengi wamebahati kupata vitu kadhaa kama baiskeli ya walemavu na hata ufadhili wa masomo kwa wale wanaosoma shuleni
Aidha Doti amesema ukubwa wa kaunti ni mojawapo ya changamoto kubwa katika kuwapa usaidizi walemavu hao.
Hata hivyo aliyekuwa mwakilishi wadi wa Sagante Adan Chukulisa ameitaka serikali kuwapa usaidizi walemavu hao kwa kuwapa hata nafasi ya ajira afisini
Baadhi ya walionufaika na usaidizi huo walishukuru serkali kwa kuwakumbuka na kuwataka kutokoma.