Watu 300 wanatarajiwa kupewa mafunzo na kujiunga na kikosi cha maafisa wa akiba NPR jimboni Marsabit.
Hii ni baada yao kupigwa msasa katika zoezi lilifanyika kuanzia wiki jana na kuongozwa na OCPD wa maeneo mbalimbali kwa ushirikiano na machifu.
Serikali itatoa mwelekeo ambapo 300 hawa watapewa mafunzo na kisha kutumwa katika maeneo mbalimbali jimboni kuimarisha usalama. Maeneo yaliyo mpakani yanatarajiwa kupewa kiapumbele ili kuzia utovu wa usalama haswa visa vya wizi wa mifugo.