KUNA HAJA YA KUAMINI UONGOZI WA AKINA MAMA KUTOKANA NA REKODI YAO YA UTENDAKAZI- WAKAAZI
November 28, 2024
Kaunti ndogo ya Moyale ndio inayoongoza kwa aina zote za saratani katika kaunti ya Marsabit kwa asilimia 52, ikifutwa na kaunti ndogo ya Laisamis kwa asilimia 37, North horr kwa asilimia 7 na Saku kwa asilimia 5.
Haya yamewekwa wazi na muuguzi anayesimamia kitengo cha matibabu ya Saratani katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Joyce Mokoro.
Akizungumza na Shajara Ya Jangwani Mokoro ameutaja mwezi wa Novemba kuwa mwezi wa kuhamasisha jamii kuhusu saratani ya mapafu huku ikiitaja kuwa sababu kuu ya vifo vinavyohusiana na saratani ulimwenguni.
Aidha Mokoro ameweka wazi changamoto ya muingiliano wa ugonjwa wa TB na saratani ya mapafu huku akitoa wito kwa jamii kujitokeza kufanyiwa vipimo ili kubaini wanachoungua mapema na kupata matibabu kwani maradhi hayo mawili yana dalili sawa.
Hata hivyo Mokoro ameutaja uraibu wa kuvuta sigara kama sababu kuu ya saratani ya mapafu, huku pia unyuaji pombe na uwepo wa kemikali zingine hatari katika mazingira zikitajwa pia kusababisha saratani hiyo katika jamii.