Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Siku moja baada Askofu mkuu wa kanisa Katoliki jimbo kuu la Nairobi Philip Anyolo kutoa taarifa ya kurudisha shilingi milioni 5 iliyochangwa na Rais William Ruto wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na kurejeshwa kwa pesa hizo.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, wamesema kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa viongozi Kanisa Katoliki.
Wametaja kwamba kanisa Katoliki limechukua uamuzi sahihi kumrudishia mchango wake rais Ruto.
Wakaazi hao wamehisi kuwa mchango wa rais Ruto ni kama hongo kwa viongozi wa Kanisa na ni njia mojawapo ya kuwanyamazisha viongozi hao wasiendelee kutetea wananchi wa Kenya..
Aidha wengine wao wametoa wito kwa viongozi wengine wa kidini kuiga mfano wake Askofu mkuu Anyolo na kujumuika kwa pamoja na kutetea mwananchi na kuwa makini wanapopokea michango hasa kutoka wanasiasa.