MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
BARAZA la mitihani ya kitaifa KNEC limetakiwa kusikiliza kilio cha walimu wanaosimamia mitihani na hata wanaosahihisha mitihani ambao kwa muda sasa wamekuwa wakiitaka serikali kuwaongezea marupurupu kwenye malipo yao.
Katibu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu KNUT tawi la Marsabit, Rosemary Talaso, ameitaka baraza hilo kusikiliza kilio cha walimu ambao wanadai kuwa malipo ya kusimamia mitihani ni kidogo ikilinganishwa na hali ngumu ya maisha ya sasa.
Wakti uo huo amepongeza serikali kwa kuwaajiri kwa njia ya kudumu walimu waliokuwa kwenye kandarasi ya muda mfupi.
Talaso ameambia radio Jangwani kuwa walimu 289 wameajiriwa na tume ya TSC katika shule za msingi na sekondari katika kaunti ya Marsabit.
Wakti uo ameomba wazazi wote walio na watoto shuleni katika kaunti ya Marsabit kuwa makini kuwalinda wana wao wakati huu wa likizo ndefu shule zitakapofungwa wiki hii na wiki ijayo. Anasema hilo litaepushia watoto uja-uzito na hata kutumbukia kwenye uovu na matumizi ya dawa za kulevya.