Raia 9 wa Eritrea na wawili Ethiopia wapigwa faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
February 24, 2025
SIKU moja baada ya kuibuka ripoti kuwa tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haitalazimishwa kupeperusha moja kwa moja matokeo ya uchaguzi wa urais yanapotangazwa na Maafisa Wasimamizi katika vituo vya kupigia kura wakaazi katika kaunti ya marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na swala hilo.
Baadhi ya waliozungumza na shajara ya radio jangwani kwa njia ya kipekee, wamesema wanapinga swala hilo wakidai ni njia mojawapo wa kuchangia kura kuibiwa na wananchi kunyimwa haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Aidha, wengine wametahadharisha matatizo yanayoweza kutokea miongoni mwa wananchi ambayo yanaweza kuathiri amani nchini.
Vile vile wengine wamedokeza njia mwafaka ambayo serikali inaweza kutumia ili kuzuia mizozo miongoni mwa wananchi na kuhakikisha kura zinapigwa kwa njia ya haki na uwazi.