Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na mapendekezo ya Senata wa kaunti ya Kiambu Karungo Thungwa ya kutaka muhula wa kutawala kupunguzwa kutoka miaka mitano hadi miaka minne.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya radio jangwani, wamesema kuwa wanaunga mkono mswaada huo wa kupunguza muda wa kuhudumu kwa viongozi wa siasa.
Wamesema kuwa miaka minne inatosha viongozi kuwahudumia Wakenya huku wakipuzilia mbali wito wa kutaka muda wa sasa wa miaka mitano kuongezwa hadi miaka saba.
Aidha wametaja kuwa uwepo wa kipindi kirefu cha kuhumu kitawafanya viongozi kulegeza kamba na kuanza kazi wakati muhula wao unakaribia kutamatika.