Local Bulletins

WAKAAZI JIMBONI MARSABIT WAHIMIZWA KUASI TAMADUNI ZILIZOPITWA NA WAKATI KAMA VILE WIZI WA MIFUGO.

Wakaazi jimboni Marsabit wamezidi kuhimizwa kuasi tamaduni zilizopitwa na wakati kama vile wizi wa mifugo.

Akizungumza na idhaa hii mapema leo asubuhi kwenye kipindi cha Amkia Jangwani, DCC wa Marsabit Central David Saruni amewataka wakaazi wanaoshirikiana na wahalifu haswa wanaotoka katika kaunti jirani kukoma.

Ijumaa wiki jana watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walivamia wafugaji katika eneo la maji la Ell Nedeni na kujaribu kuiba mbuzi zaidi ya 100 ambao waliweza kurejeshwa na maafisa wa polisi waliofika katika eneo hilo.

Uvamizi huo ulitekelezwa na majambazi kutoka kaunti jirani

Na kutokana na visa vya wizi wa bodaboda humu mjini Marsabit Saruni amewataka wahudumu wa bodaboda kuchukua tahadhari na pia kushirikiana.

Aidha Saruni amedokeza kuwa watazidisha doria viungani mwa mji wa Marsabit kutokana na kuongezeka kwa visa vya wizi ambapo maduka yanavunjwa na kuporwa.

Subscribe to eNewsletter