Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Wahamiaji haramu 23 raia wa Eritrea wamefikishwa katika mahakama ya Marsabit kwa mashtaka ya kupatikana nchini bila shtakabadhi za kuwaruhusu kuwa nchini.
Wahamiaji hao walikamatwa na maafisa wa polisi katika eneo la manyatta Karatasi eneo bunge la Saku Kaunti hii ya Marsabit.
Miongoni mwa wahamiaji hao ni wanaumme 19 na wanawake wanne.
Walikifikishwa mbele ya hakimu mkuu mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Christine Wekesa kujibu mashtaka. Wote walikiri mashtaka dhidi yao
Hakimu Wekesa kupitia hukumu ya njia video aliwapata na hatia wahamiaji hao na kuwapiga faini elfu Arobaini au kifungo cha miezi mitano na kila mmoja