Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Ni watu wachache sana walioelewa jinsi ya kutumia fedha zao ipasavyo.
Haya ni kwa mjibu wa mataalam wa maswala ya kifedha John Maina.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Maina amesema kuwa watu wengi wanapata pesa ila wanaojua namna ya kuzitumia vyema ni wachache mno huku akiweka wazi kuwa utumizi wa pesa inavyostahili unategemea tabia ya mtu binafsi.
Aidha Maina amekariri hoja ya wafanyikazi kuwekeza fedha zao katika miradi inayoleta faida na pia kuweka akiba kwa ajili ya siku za usoni.
Amewashauri wafanyikazi kujiepusha na matumizi mabaya ya fedha huku akitaja kwamba baadhi ya mambo yanayotumia fedha nyingi kama vile burudani yanaweza epukika.
Hata hivyo mataalam huyo wa maswala ya kifedha amewaraia watu kuishi kulingana na kipato chao ili kuepuka mzigo mkubwa wa maisha.