Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Afisa anayesimamia usafi wa chakula katika kaunti ndogo ya Saku Goba Boru amewaonya wale wale wanaozugusha vyakula mitaani katika kaunti ya Marsabit kuwa wakabiliwa kisheria.
Akizungumza na Radio Jangwani, Boru amesema kuwa zoezi la uchuuzi wa chakula ni kinyume cha sheria kwani vingi vya vyakula hivyo vinavyozungushwa mtaani havijafikia vigezo vya usafi.
Aidha Boru amewashauri wamiliki wa hoteli na bucha kuzingatia usafi la sivyo watakabiliwa kisheria.
Hata hivyo amehimiza wakaazi wa Marsabit kujitahadhari na vyakula vinavyozungushwa mtaani ili kujiepusha na maradhi kama vile kuendesha.