Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kujikinga na baridi ili kujiepusha na magonjwa yanayosababishwa na baridi.
Haya ni Kwa mujibu wa Bonsa Doti ambaye ni muuguzi wa afya katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani afisini mwake, Doti amesema kuwa ni muhimu kujizuia baridi kwa kuvaa mavazi mazito ili kujiepusha na hatari za kuugua.
Aidha, Doti amesema kuwa, msimu huu wa baridi idadi ya wagonjwa wanaoathirika kutokana na magonjwa kama vile asthma na bronchitis inaongezeka.
Zaidi ya hayo amewataka watu wanaougua ugonjwa wa asthma wajikinge zaidi msimu huu wa baridi.