Aliyekuwa meneja wa Tume ya Haki na Amani (CJPC) katika shirika la Caritas Marsabit Gabriel Gambare azikwa katika eneo la Hula Hula.
November 12, 2024
Visa vya utapiamlo vimeongeka hadi asilimia 15.2 kutoka 13.5 katika kaunti hii ya Marsabit.
Ongezeko hili likiwa ni kutoka mwezi wa Julai hadi mwezi septemba mwaka huu kulingana na deta za mamlaka ya kukabiliana na ukame NDMA.
Kulingana na afisa mkuu wa lishe bora katika kaunti ya Marsabit David Buke, watoto walio na umri wa miezi 6 hadi miaka 5, kina mama wajawazito, watu wanaoishi na magonjwa sugu pamoja na wazee katika jamii ndio wameathirika zaidi.
Buke anasema kuwa maeneo ambayo yameathiria pakubwa ni pamoja na Marsabit ya kati, wadi ya Golbo, Loiyangalani kati ya maeneo mengine jimboni.
Buke amesema kuwa hili linatokana na ugumu wa maisha unaotokana na hali ya uchumi ulivyo kwa sasa.
Vievile ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto hospitalini ili kupata msaada wa virutubishi vya aina mbalimbali.
Buke ametoa wito wa ushirikiano kutoka kwa washkadau mbalimbali kunusuru jamii kutoka kwa hali hii ya utapiamlo.