MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Na Carol Waforo
Visa vya ulawiti (sodomy) vimeongezeka pakubwa katika eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.
Haya ni huku taifa likiendeela kuadhimisha mwezi wa huduma kwa watoto katika mwezi huu wa Novemba.
Kulingana na afisa wa watoto katika shirika la Strategies for Northern Development SND Joan Chebet aliyezungumza na shajara ya Radio Jangwani ni kuwa hili limechangiwa na pengo lililopo wakati jamii inapigania haki za mtoto wa kike.
Na huku jamii ikielewa kwa upana madhara ya dhulma dhidi ya mtoto wa kike afisa huyu anasema kuwa ipo haja kubwa ya jamii kuelimishwa zaidi kuhusiana na madhara ya kukiuka haki za mtoto wa kiume.
Na kando na visa vya ulawiti pia imebainika kuwa visa vya dhulma za aina nyingine kwa watoto vimeongezeka.
Joan anasema kuwa kwa sasa kuna kesi zaidi ya 26 mahakamani zinazofungamana na dhulma dhidi ya watoto nyingi ya kesi hizo zikiwa za unajisi huku shirika la SND likifanya kazi kwa ukaribu na mahakama kuhakikisha kuwa watoto wale wanapata haki.
Na huku watoto wakisalia nyumbani kwa likizo ndefu afisa huyu wa watoto anasema kuwa pia visa vya ulanguzi wa watoto vimeongezeka katika eneo bunge hilo la Moyale.
Licha ya haya watu wanaojitokeza katika kuripoti visa hivi pia imeongezeka na ambayo inakuwa ni hatua kubwa katika kukabiliana nazo.
Na huku kaunti ya Marsabit ikijiunga na Taifa nzima katika kuadhimisha siku ya wanaume ulimwenguni Joan anasema kuwa ipo haja kubwa ya jamii kupigania haki za mtoto wa kiume na kuwawezesha sawa na wale wa kike.