MOHAMED NANE AMEWEKA WAZI SABABU YA KUSUSIA UCHANGUZI WA LEO.
November 14, 2024
Viongozi wa Marsabit wameshauriwa kuhamasisha umma kuhusu rasilimali asili zinazopatikana hapa jimboni.
Viongozi katika kaunti ya Marsabit wameshauriwa kuhamasisha umma kuhusu rasilimali asili zinazopatikana hapa jimboni. Haya ni kwa mujibu wa mshauri wa Kiutawalawa shirika la NAPO Dr Elizabeth Pantoren
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Pantoren amesema kuwa wakazi katika kaunti ya Marsbit hawana uelewa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali na pia jukumu lao katika kutunza na kuhifadhi rasilimali ambazo ndio kivutio cha utalii jimboni.
Pantoren ameelezea kuwa ni haki ya kila mwanaMarsabit kupata taarifa muhimu kuhusu rasilimali ambazo zinapatikana katika kaunti ya Marsabit akisema kuwa hii itasaidia katika kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa misitu, wanyamapori na hata mbuga zote za Marsabit
Kadhalika amesema kuwa ili kupunguza migogoro inayoshuhudiwa kuhusu umiliki wa rasilimali ni sharti kila mmoja awe na uelewa kuwa umiliki wa rasilimali mbalimbali zinazopatikana hapa jimboni.