Levaquin: Comprehensive Guide on Usage, Benefits, and Safety
December 20, 2024
Muaniaji wa nafasi ya mwenyekiti wa shirilikisho la mpira wa miguu FKF tawi la Marsabit Godana Roba Adi amekanusha madai kuwa amewashawishi wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya Simu, Godana ametaja kwamba amefuata mikakati yote inayofaa katika kusaka uungwaji mkono kwenye kinyanganyiro hicho huku akilitaja swala la kuwashawishi wapiga kura kama lisilo na misingi yeyote.
Godana amewarai wapiga kura kuwa subira kuhusiana na siku ya kupiga kura baada ya mahakama ya Kitui, ijumaa wiki jana kusitisha zoezi la uchaguzi ambalo lilifaa kufanyika jumamosi wiki jana.
Aidha Godana ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa katika nafasi hiyo, atahakikisha kwamba ligi ya kabumbu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu kaunti ya Marsabit inafufuliwa.
Vilevile amekanusha madai kwamba anatumiwa au kupendelewa na serekali ya kaunti ya Marsabit ili kuhakikisha kwamba anaendeleza ajenda zao iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo la mpira wa miguu.
Hata hivyo Godana ameunga mkono swala la sekarekali kuwekeza katika mafunzo ya kabumbu katika kila eneo bunge akitaja kwamba hilo litasaidia kukuza talanta.