Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Huku ulimwengu ukisherekea siku ya Ugonjwa wa Sukari, ugonjwa huu umetajwa kama mmoja wa magonjwa yanayochangia kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa figo.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, muuguzi wa figo katika Hospitali ya Rufaa ya Marsabit, Abdinassir Mohamed Jillo, amesema kuwa ugonjwa wa figo umeenea kati ya vijana wadogo hapa Marsabit.
Aidha, Mohamed ametaja sababu ambazo zinachangia wagonjwa kupata ugonjwa wa figo ni pamoja na ugonjwa wa sukari usiothibitishwa, shinikizo la damu, matumizi ya dawa kwa muda mrefu bila idhini ya daktari, matumizi ya dawa za kienyeji, sawa na maswala mengineyo.
Hata hivyo Mohamed amewahimiza wakaazi kutembelea hospitali ili kupima sukari na shinikizo la damu, na kupunguza matumizi ya dawa kiholela.