Wafugaji jimboni Marsabit wahimizwa kuwapeleka wanao shuleni.
January 24, 2025
Utafiti uliofanywa kuhusu ugonjwa wa maziwa (brucellosis) kati ya mwaka 2013 hadi sasa, na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani katika kaunti ndogo ya Laisamis, umebaini kwamba ugonjwa huu upo kwa kiwango cha juu miongoni mwa wanyama na binadamu.
Akizungumza na radio Jangwani kwa njia ya simu, Mkurugenzi Msimamizi katika Idara ya Mifugo, Daktari Boru Botha, amesema kuwa wakaazi wanapaswa kuwa waangalifu wanapotumia bidhaa za mifugo kama maziwa na nyama.
Boru amesema ugonjwa huu unachochewa na matumizi ya nyama na maziwa ambayo hayajatunzwa vizuri. Aidha, alitaja njia nyingine ambazo ugonjwa huu unaweza kuenezwa, ikiwemo kula na mizoga ya wanyama kwa njia isiyofaa.
Hata hivyo, Botha amehamasisha wakaazi kwamba njia bora ya kujiepusha na ugonjwa huu ni kuchemsha maziwa, kutumia glovu wanaposhughulika na mizoga ya wanyama, kupika nyama vizuri, na kuepuka mila potofu kama vile kunywa maziwa yasiyochemshwa. Pia amesisitiza umuhimu wa kutembelea hospitali mara kwa mara ili kupata matibabu.