Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Wazazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuhakikisha kwamba wamewapeleka wanao shuleni ili wapate elimu wakati wapo katika umri wa kusoma.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit ni kwamba ni changamoto kwa wengi kusoma wakiwa watu wazima jambo linaloweza kuadhiri masomo yao.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake baada ya kukamilika kwa mitihani ya kitaifa KCSE, Magiri ametaja kwamba idara hiyo pamoja na watahiniwa wa kibinafi 154 ambao wamekalia mtihani wa KCSE mwaka huu wamepitia changamotio si haba wakati wa mitihani jambo ambalo lingeipukika iwapo wananchi hao wangeapata elimu wakiwa wachanga.
Aidha Magiri ameweka wazi kwamba mtihani wa kitaifa KCSE mwaka huu umekamilika vyema bila changamoto nyingi kutokana na mikakati iliyowekwa na baraza la mitihani nchini KNEC kuzuia wizi wa mitihani.
Hata hivyo Magiri amesifia hatua ya kuwabadilisha waangalizi wa mitihani kila wiki akitaja kwamba hilo limesadia pakubwa kuhakikisha kwamba mitihani hiyo inakamilika bila visa vya wizi kuripotiwa.