Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Wafanyikazi wa kujitolea katika eneo bunge la Saku wametishia kususia kuwasilisha ripoti za kazi wanazofanya vijijini hadi pale watakapolipwa mishahara yao.
Kwa mujibu wa kiongozi wa wafanyikazi hao kutoka hapa mjini Marsabit Rashid Abdi ni kuwa watatumia hilo kama njia ya kushikiza serekali ya kaunti ya Marsabit kushughulikia maswala ambayo yanawaadhiri ikiwemo ukosefu wa mishahara.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia kipekee, Rashid amelalama kwamba hawajapokea mishahara ya miezi minee ambayo ni mwezi Julai, Agosti, Septemba na Oktoba jambo linalolemaza utendakazi wao.
Kando na hilo Rashid anahoji ni vipi baadhi ya wafanyikazi wa kujitolea CHPs hapa jimboni Marsabit hawapokea malipo pia kutoka kwa serekali ya kitaifa, huku akiitaka idara husika kushughulikia hilo na kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata haki yake.
Rashid vilevile amelalamikia kile amekitaja kwamba ni kubaguliwa kwa baadhi ya maafisa wa afya wa kujitolea CHPs wakati wa kutolewa kwa mafunzo kwani ni wachache tu ndio huchaguliwa ili kupata na pia wao hulazimika kutoa hongo kwa afisa mmoja wa kaunti ili kupata nafasi hizo.