Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Mashindano ya Muziki ya Watoto wa PMC yameanza rasmi leo katika Kanisa Katoliki la Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii, Andrew Abdub ambaye ni mwenyekiti wa parokia, amesema kuwa vigango vinne vitashiriki katika tamasha hilo. Alisisitiza kwamba lengo la mashindano ya leo ni kutafuta washiriki watakaowakilisha dayosisi ya Marsabit katika tamasha la muziki.
Aidha, Padre Paul Makokha, padre wa parokia ya kanisa katoliki la marsabit cathedral, amesema kwamba madhumuni ya tamasha hili ni kuwaleta watoto pamoja ili washiriki, kujuana, na pia kuwasaidia watoto kuepuka maadili mabaya.
Wakati uo huo Padre Makokha amewaomba wazazi kuchukua jukumu katika kuwalea watoto wao. Aliwarai wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao wakati huu wa likizo ndefu.