Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Tutawakamata wazee ambao wataendeleza ndoa za mapema katika eneo la Loiyangalani.
Haya ni kwa mujibu wa naibu kamishna wa eneo la Loiyangalani Stanley Kimanga.
Kimanga amesema kuwa ni jukumu la wazee kulinda haki ya mtoto msichana na kuwaepusha na mila potovu ambayo imepitwa na wakati.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Kimanga amesema kuwa wasichana waliopata mimba wakiwa shuleni ni sharti warejeshwe shuleni ili kupata haki yao ya elimu akisema kuwa yeyote atakayepatikana amekiuka hili atakamatwa na kushtakiwa kulingana na sheria.
Kimanga hata hivyo amesifia hatua ambayo idara ya usalama imepiga katika kuleta utulivu Loiyangalani akishukuru ushirikiano uliopo baina ya wakazi wa eneo hilo na maafisa wa polisi.
Kadhalika Kimanga amesema kuwa bado wanashirikiana na washikadau tofauti kuhakikisha kuwa wameboresha barabara ya Loiyangalani ambayo imeharibiwa na kujaa kwa maji ya ziwa Turkana.