MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kumaliza umaskini duniani,serekali ya kaunti ya Marsabit pamoja na ile ya kitaifa zimetakiwa kuwapiga jeki vijana na wanawake haswa walio katika sekta ya kilimo ili kupunguza kiwango cha umaskini katika kaunti ya Marsabit.
Kulingana na mkurugenzi wa shirika la maendeleo endelevu, Initiative for Progressive Change (IFPC) Hassan Mulata ni kuwa kiwango cha umaskini katika kaunti ya Marsabit bado kipo juu kwani asilimia 65.9 bado wanaishi na umaskini.
Akizungumza na Idhaa hii kwa njia ya kipekee Mulata ametaja kwamba iwapo wananchi wataweza kujilisha basi itakuwa rahisi kupunguza umaskini hapa jimboni Marsabit.
Aidha Mulata ameitaja hali ya ukame sawa na ukosefu wa amani katika kaunti ya Marsabit kama sababu kuu ambazo zimepelekea kiwango cha umaskini kuongezeka.
Hata hivyo Mulata amesikitikia kile amekitaja kwamba ni idadi kubwa ya watu wanaoishi na umaskini mijini ikilinganishwa na wale wanaoishi mashinani.