Local Bulletins

ONYO KALI IMETOLEWA KWA WALANGUZI WA MIHADARATI NA DAWA ZA KULEVYA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT.

Onyo kali imetolewa kwa walanguzi wa mihadarati na dawa za kulevya katika kaunti ya Marsabit.

Kwa mujibu wa kamishina wa kaunti ya Marsabit James Kamau ni kuwa watakaopatikana wakiuza au kusafirisha mihadarati katika kaunti ya Marsabit watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake, kamishina Kamau amesema kuwa mikakati kabambe imewekwa kuhakikisha kwamba mihadarati haisafirishwi hapa jimboni kupitia mpaka wa taifa jirani la Ethiopia.

Aidha kamishina Kamau amewataka wazazi kufuatilia mienendo ya wanao haswa kipindi hichi cha likizo ili kuwazuia kujiingiza katika utumizi au biashara ya mihadarati.

Mkuu huyo wa usalama jimboni ameweka wazi kuwa hatua kadhaa zimewekwa ikiwemo ukaguzi wa kina katika vizuizi vya barabarani sawa na ushirikiano na idara ya mahakama ili kuhakikisha kwamba biashara ya mihadarati haisheni hapa jimboni.

Kuhusuana na mihadarati ambayo hushikwa katika kaunti jirani na kusemekana kwamba imepitishwa jimbo la Marsabit, kamishna Kamau amekariri kuwa walangunzi muda mwingine hutua vichochoro na kuhepa barabara kuu ya Marsabit – Isiolo ili kukwepa polisi.

Subscribe to eNewsletter