Aliyekuwa meneja wa Tume ya Haki na Amani (CJPC) katika shirika la Caritas Marsabit Gabriel Gambare azikwa katika eneo la Hula Hula.
November 12, 2024
Mashirika yasiyo ya kiserikali yamehimizwa kuwasaidia watoto wakati wa likizo kwa kuandaa mchezo ili kusaidia watoto wajiepushe na mihadarati.
Akizungumza na idhaa hii Evana Esokon ambaye ni msimamizi wa shirika la Loyangalani Spring Of Hope ni kuwa wakati wa likizo ndefu watoto wengi wanajihusisha na mambo ambayo hayafai kama vile mihadarati na mimba za mapema hivyo mchezo huo utasaidia kuwaleta watoto pamoja ili kuvipunguza visa hivi.
Aidha Esekon amewahimiza wazazi kuwachunga wanao wakati huu wa likizo ndefu akisema kuwa eneo kama Loyangalani lina ziwa ambayo ni hatari kwa watoto wakati huu ambao mvua umeanza kunyesha.
Esokon ameomba wazazi kuwalinda watoto wao dhidi ya dhulma za kinjisia akisema kuwa wazazi wengi hupuuza miendo ya watoto wao.
Wakti uo huo Esekon amewaomba pia wahisani kuwasaidia wasichana waliopata mimba za mapema kurejeshwa shule ili waweze kupata elimu.