Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Mwanaume moja mwenye umri wa miaka 27 amehukumiwa kifungo cha miaka 10 kwa jaribio la ubakaji katika mahakama ya Marsabit.
Mahakama imempata na hatia baada ya kuarifiwa kuwa mnamo tarehe 15 Januari mwaka 2024 katika eneo la manyatta Sessi eneobunge la Northhorr kaunti ya Marsabit mtuhumiwa Shuna Wario Halakhe alijaribu kumnajisi msichana wa miaka 15.
Mshukiwa alikammatwa tarehe 15 mwezi Januari na kufikishwa mahakamani tarehe 17 mwezi uo huo.
Kesi hiyo imekuwa ikiendelea ambapo hapo jana Alhamisi tarehe 24 hakimu mwandamizi Simon Arome alimhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani.
Mshukiwa ana siku 14 kukata rufaa.
Wakati uo huo
Mwanaume moja amefikishwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kumbaka mwanadada moja na kumpachika mimba.
Mahakama ya Marsabit imearifiwa kuwa mnamo tarehe 28 mwezi Septemba mwaka 2023 katika eneo la shrine wadi ya Marsabit central eneobunge la Saku kaunti ya Marsabit mshukiwa Ware Bolasa Hase alitekeleza kitendo hicho.
Mshukiwa alikamatwa tarehe 21 mwezi huu wa octoba mwaka 2024 na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 22 mwezi huu mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome.
Mshukiwa amekana shtaka na kuachiliwa na dhamana ya shilingi 100,000.
Mahakama aidha imeamuru uchunguzi wa msimbojeni DNA kufanyika ukihusisha mwathiriwa, mwanawe na mshukiwa.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 28 mwezi huu wa Octoba 2024.