Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Mifugo katika lokesheni za Balesa, Dukana na El Adhe Eneobunge la North Horr huenda ikakumbwa na ukosefu wa lishe baada ya moto unaosambaa kwa kasi kuteketeza sehemu kubwa ya malisho.
Chifu wa Dukana Tuye Katello ameambia shajara kuwa moto mkubwa ulioanzishwa na mfugaji mmoja umeenea kwa kasi kutokana na wingi na ukavu wa nyasi.
Moto huo ulioanza saa sita mchana siku ya Alhamisi na kuenea katika lokesheni hizo tatu anasema umekuwa na changamoto kuzimwa licha ya juhudi ambazo wakazi wamefanya kufikia sasa.
Licha ya kuhakikisha kuwa ajali hiyo si kisa cha kimakusudi amesema kuwa ni vyema kila mmoja haswa wafugaji kuwa makini na hatari ya moto kwani athari zake ni kubwa ikizingatiwa kuwa ni nyasi zizo hizo ndizo zinategewa na mifugo.
Sio mara ya kwanza mioto kuanzishwa na wafugaji katika eneobunge la North Horr visa ambavyo kwa upana uathiri lishe ya mifugo haswa panapotokea kiangazi ya kupindukia.
ReplyForward |