Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu tawi la Marsabit Mohamed Nane ameweka wazi kuwa amesusia uchanguzi wa leo kutokana na mpinzani wake kuwashawishi wapiga kura kwa misingi ya kikabila.
Nane ambaye hakuwasili katika ukumbi wa uchanguzi wala kutuma ajenti wake ametaja kwamba mpizani wa Godana Roba Adi amewashawishi wapiga kura kwa kutumia wazee wakuwatisha kwa misingi ya kikabila.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia simu Mohamed Nane ametaja kwamba amefedheheshwa na swala la ukabila kuingizwa katika uchaguzi mkuu wa FKF mwaka huu kaunti ya Marsabit, huku akiahidi kwamba atakabidhi mamlaka kwa Godana Roba Adi iwapo atatangazwa mshindi.
Aidha Nane ameahidi kushirikiana na upande wa Godana Roba japo amesisitiza kwamba, swala la michezo katika kaunti ya Marsabit lililemazwa na serekali ya kaunti ya Marsabit idara ya michezo.