Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Visa vya mimba za mapema vimetajwa kuwa sababu kubwa ya wasichana kukosa kwenda shule kote nchini kwa aslimia 39.2% huku asilimia 27.3% ikikosa kwenda shule kutokana na ukosefu wa karo.
Kaunti ya Marsabit imetajwa pia kuwa kaunti mojawapo ya kaunti inayoshuhudia asilimia kubwa ya wanafunzi wasiohudhuria masomo kuanzia madarasa ya chekechea hadi shule za upili kutokana na sababu nyingi ikiwemo kutopikwa shuleni.
Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Marsabit Peter Magiri ameambia shajara kuwa kijumla wanafunzi wa shule za madarasa ya chini Marsabit wanachochewa kwenda shule na uwepo wa lishe shuleni.
Kero nyingine inayochangia watoto kutokwenda kulingana naye ni ukosefu karo na kutegemea pakubwa misaada ya basari au wafadhili.
Ndoa za mapema, kuhamahama na kutoona umuhimu wa masomo.
Suala la mila na desturi ya kuoa wasichana wadogo pia imetajwa kama kikwazo kikuu kaunti ya marsabit suala ambalo afisa huyo wa elimu ametaja kuwa jamii inafaa kuelimishwa.