Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Jamii ya Marsabit imetakiwa kuasi mbinu za kukata miti na kuchoma makaa ili kuzuia uharibifu zaidi wa mazingira.
Kwa mujibu wa mshirikikishi wa maswala ya kawi katika kaunti ya Marsabit Joseph Agola ni kuwa jamii inafaa kuwa makini na matumizi ya makaa na kuni ili kuzuia uharibifu zaidi wa mazingira unaosababisha mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisini mwake Agola ametaja kwamba ipo hoja ya jamii ya Marsabit kukumbatia mbinu mbadala ya upishi kama vile jiko za kisasa ambazo haziharibu mazingira kwa kiwango kikubwa.
Aidha Agola amesema kuwa mikakati ya kuhakikisha kwamba kampuni ya kutengeza jiko hizo za kisasa katika eneo la Ngurunit imewekwa ili kuhakikisha kwamba zinafika katika kila pembe ya kaunti ya Marsabit.
Na licha ya kaunti ya Marsabit kuwa na idadi kubwa ya mifugo, Agola ametaja kwamba itakuwa vigumu kwa mfumo wa kawi wa Biogas kufaulu kutokana na zoezi la wafugaji kuhamahama.
Ametoa wito kwa jamii kupanda miti na kutunza iliyopo ili kuepusha uharibifu zaidi wa mazingira.