Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Hali ngumu ya uchumi imechangia changamoto wanayopitia wanawake katika kaunti ya Marsabit ambayo inasababisha mavurugano katika familia. Haya ni kwa mujibu wa mtetezi wa haki za kibinadamu kutoka shirika la MWADO, Dale Ibrahim.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Dale amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa imechangia pakubwa uwepo wa migogoro miongoni mwa wanawake kaunti ya Marsabit.
Pia ametaja kuwa asilimia kubwa ya watoto wanapitia dhuluma kama vile ukeketaji na ndoa za mapema.
Aidha Mary Nasibo ambaye pia ni mtetezi wa haki kutoka shirika hilo la Mwado amesema kuwa wanachukua hatua mwafaka ya kuwalinda wanawake na pia watoto kutokana na dhuluma za kijinsia.
Wawili hao wametoa wito kwa wazazi katika kaunti ya Marsabit kuwalinda watoto haswa wakati huu wa likizo wa mwezi disemba.
Wamehimizwa wajue mambo wanayojihusisha wanao .
Pia wazazi wameonywa dhidi ya kuwaoza na kuwa keketa wasichana msimu huu wa disemba.