MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
NAIBU kamishna wa kaunti ndogo ya Laisamis Kepha Maribe amesema elimu pekee kwa jamii za Marsabit ndio suluhu mwafaka ya kumaliza kero la wizi wa mifugo ambao hushuhudiwa mara nyingi katika eneobunge hilo.
Maribe akizungumza na shajara ya Radio Jangwani amesema kuwa serikali chini ya uongozi wake utahakikisha kuwa watoto wote wa kaunti ndogo ya Laisamis wanapokea elimu ili iweze kuwafaa siku za usoni sawa kukomesha utamaduni wa wizi wa mifugo.
Amesema kuwa ataomba baraza la wazee wa kijamii kuhakiki upya utamaduni wa kutahiri wavulana ambao unachukua muda mrefu kitu anachodai inachangia kukuza utamaduni wa wizi wa mifugo uliopitwa na wakati.
Kauli yake DCC Maribe inajiri wiki kadhaa baada ya ngamia wanaodaiwa kuibiwa kutoka kaunti za isiolo na Samburu kupatikana katika kaunti ndogo ya laisamis. Mifugo mingine iliweza kuibiwa kaunti ya isiolo hapo maajuzi na na inadaiwa kuelekezwa kaunti ya Marsabit.
Kuhusiana na uwepo wa kiangazi kamishna Maribe amesema hadi sasa serikali inasaidia kwa kuwapa wananchi chakula kidogo ili kuzima njaa ambayo inaendelea kushuhudiwa sehemu kadha za Marsabit.