Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
Siku chache tu baada ya kiongozi wa wahuduma wa afya wa kujitolea kutoka mjini Marsabit Rashid Abdi kulalamikia kile alikitaja kuwa baadhi yao viongozi katika idara ya afya wanawaidai hongo ili kuwaruhusu kuhudhuria mafunzo mbalimbali,sasa kiongozi huyo ametaja kuwa ametishiwa kufutwa kazi kutokana na kauli yake.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia kipekee, Rashid ametaja kwamba aliitwa ofisini na msimamizi wa wahudumu wa afya wa nyanjani CHPs katika eneo bunge la Saku Abdulahi Konsole na kutishiwa kufutwa kazi kutokana na kile Konsole alikitaja kwamba ni kuvunja sheria.
Aidha Rashid ameyataja maneno ya Konsole kama vitisho vinavyolenga kuadhiri utendakazi wake kwani bado hajapewa barua ya kusimamishwa kazi.
Kadhalika Rashid ametetea hatua yake ya kutoa lalama kwa vyombo vya habari kwani hilo lilisadia wao kulipwa mishara yao ya miezi mitatu ambayo walikuwa wanadai.
Hata hivyo ametoa wito kwa usimamizi wa idara ya afya kuhakikisha kwamba wanatatua maswala yanayowadhiri wafanyikazi wa kujitolea hapa jimboni bila vitisho vyovyote.
Kwa upande wake msimamizi wa wahudumu wa afya wa nyanjani CHPs katika eneo bunge la Saku Abdulahi Konsole ambaye aliongea na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya simu amedhibitisha kwamba ni kweli wanapanga kuwasilisha lalama zao kwa wazee na kuhakiskisha kwamba wanatoa mtu mwingine kuhudumu katika nafasi ya Rashid Abdi japo hakutaka sauti yake kutumika hewani.
Konsole amekanusha madai kwamba uamuzi wa kumfuta kazi Rashid haujaafikiwa baada yake kupeleka malalamishi yake kwa vyombo vya habari mbali ni kutokana na rekodi ya utovu wa nidhamu ambapo alikuwa ameonywa mara mbili hapo awali.
Japo amekanusha madai kuwa maafisa hao wanyajani walilipwa mishahara yao ya miezi mitatu ambayo wamekuwa wakilalamikia baada ya Rashid kulalama, Konsole ameweka wazi kuwa mafiasa hao wa nyajani wameshalipwa mishahara yao ya hadi mwezi Oktoba mwaka huu huku akiwataka kufuata njia zinazohitajika kuwasilisha malalamishi yao badala ya kupeleka kwa vyombo vya habari.
Vile Konsole ameahidi kuwa lalama kuhusu wahudumu hao wa nyajani kuitishw ahongo ili kuhudhuria mafunzo yatachunguzwa kwani hakuna yeyote anayefaa kutoa hongo ili kupata mafunzo kuhusiana na namna ya kuboresha utoaji huduma kwa jamii.