Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Idara ya barabara kaunti ya Marsabit itahakikisha kwamba inakarabati barabara zitakazoharibiwa na mvua inayoshuhudiwa katika maeneo mengi ya jimbo la Marsabit.
Haya ni kwa mujibu Dr Hitler Rikoi ambaye ni afisa mkuu kutoka idara ya barabara kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake Hitler ametaja kwamba licha ya mvua inayozidi kushuhudiwa hapa jimboni,idara ya barabara itahakikisha kwamba zoezi la usafiri halitatiziki kamwe.
Kuhusiana na barabara ya Nyayo road wadi ya Marsabit ya Kati barabara ambayo imeibua malalamishi katika siku za hapo nyuma kutokana na ubovu wake, Hitler amelaumu wakaazi wanaoishi kando ya barabara hiyo kwa kukosa kushirikiana na idara ya barabara.