Levaquin: Comprehensive Guide on Usage, Benefits, and Safety
December 20, 2024
Baraza la watu wanaoishi na ulemavu limeadhimisha miaka 20 tangu kuadhimishwa kwake huku jumbe za kuwajali walemavu zikisheheni wakati wa maadhimisho hayo hapa jimboni Marsabit.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya huduma za jamii katika kaunti ya Marsabit Galgallo Okata ni kuwa serekali ya kaunti ya Marsabit imehakikisha kwamba watu wanaoishi na ulemavu wanapata haki zao za kimsingi.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani baada ya mkao wa kuadhimisha miaka 20, Okata amesema kuwa pia serekali ya kaunti kwa ushirikiano na serekali kuu imehakikisha kwamba walemavu wamesajili na kupata fedha za mkoba wa INUA JAMII.
Okata ameweka wazi kuwa serekali ya kaunti inahakukisha kwamba majengo yanayojengwa yanajengwa kwa namna ambayo itawawezesha walemavu kuingia ili kupata misaada mbalimbali.
Kadhalika ameitaka jamii kutowatenga katika kufanya maamuzi kwani pia wao wanafaa kuwa na usemi katika miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Hata hivyo Okata ameitaja changamoto ya ukubwa wa kaunti ya Marsabit kama mojawepo ya maswala yanayolemaza utoaji huduma kwa watu wanaoishi na ulemavu.
Vilevile amewataka wananchi kutowaficha watu wanaoishi na ulemavu na badala yake kuhakikisha kwamba wamepata haki ya elimu ili kujifaidi katika maisha yao ya usoni.