MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Na Isaac Waihenya & Abdilaziz Abdi,
Badhii ya manahodha wa vilabu vya kabumbu katika eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni kufungiwa nje kwenye uchaguzi mkuu wa kuwachagua viongozi wa michezo katika jimbo la Marsabit
Wakizungumza na waadishi wa habari hapa mjini Marsabit manahodha hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Siba Bulcha ambaye pia na nahodha wa klabu ya Samba, wamesema kuwa mwenyekiti wa sasa Mohamed Nane amewasilisha orodha ya vilabu 10 pekee vitakavyoruhusiwa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu huo ujao licha kuwa kuna vilabu 60 hapa jimboni Marsabit.
Aidha Bulcha amekariri hoja ya serekali ya kaunti na viongozi wengine kuangazia swala la michezo kuona kwamba hakujakuwa na ligi ya kabumbu tangu mwaka wa 2019.
Waimeitaka idara ya michezo nchini kuingilia kati na kuhakikisha kwmaba ujenzi wa uwanja wa Marsabit unakamilika.
Kauli yake imeungwa mkono na nahodha wa timu ya Fabich Dofa Mamo ambaye amekariri kuwa hata licha ya baadhi ya vilabu kujisajili kwa shilingi elfu 6 ili kupata vyeti na vitambulisho mwaka mmoja uliopita,bado ofisi ya Mohamed Nane imeshikilia stakabadhi hizo, swala ambalo linalemaza maendeleo ya vilabu.
Hata hivyo manahodha hao wamemtaka mbunge wa Saku Dido Ali Raso pamoja na wabunge wengine katika kaunti ya Marsabit kuelekeza mgao wa asilimi 2 ya hazina ya NGCDF ambao umetengewa michezo ili kuhakikisha kwamba vijana wanajihusisha katika michezo na kuwaepusha na utumizi wa mihadarati na dawa za kulevya.