Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Asilimia 47.9 ya kaya katika kaunti ndogo ya Saku zinamiliki vyoo na kuvitumia katika kuzuia utupaji wa kinyesi ovyo maarufu Open Defecation Free (ODF)
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa afya katika kaunti ndogo ya Saku Gobba Boru.
Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya usafi wa mkono duniani iliyoandaliwa katika zahanati ya Jirime,kaunti ya Marsabit, Gobba amesema kuwa ni kaya 92 ambazo zinamiliki vyoo katika kaunti ndogo ya Saku, kaya 3 zikiwa katika wadi ya Karare, 52 katika wadi ya Marsabit Central na 37 katika wadi ya Sagante Jaldesa.
Gobba amekariri hoja ya kuwapongeza wahumudu wa afya ya jamii pamoja na wahudumuwa wa afya wasaidizi kwa majukumu yao ya kuhakikisha kuwa maeneo mengi katika kaunti ndogo ya Saku yamedumisha usafi.
Afisa huyo amewataka wakazi wa kaunti ya Marsabit kukumbatia mtindo wa kuosha mikono mara kwa mara ili kujizuia na magonjwa yanayotokana na uchafu.