Levaquin: Comprehensive Guide on Usage, Benefits, and Safety
December 20, 2024
Afisa mkuu katika idara ya utamaduni na jinsia kaunti ya Marsabit Anna Maria Denge amewapongeza Arbe Roba Gocha na Leah Lesila ambao walipeperusha bendera ya Marsabit kwenye mashindano ya watu wanaoishi na ulemavu ya Nondo Desert Wheel Chair yaliyoandaliwa mnamo siku ya jumamosi katika kaunti ya Isiolo.
Arbe Roba Gocha alichukua nafasi ya 3 katika mashindano ya watu wanaoishi na ulemavu ya Nondo Dersert Wheel Chair race upande wa wanawake huku Leah Lesila akichukua nafasi ya pili katika mashinano ya urembo upande wa wanawake.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Anna Maria amewapongewa wote waliowakilisha jimbo la Marsabit katika mashindano hayo huku akiwarai kutia bidii ili kufanya vyema zaidi katika mashindano ya mwaka ujao.
Hata hivyo Anna Maria ametoa wito kwa jamii kutowaficha watu watoto wanaoishi na ulemavu na badala yake kuwapeleka shuleni ili wapate elimu itakayowafaidi katika siku za usoni.