Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Risala za rambi rambi zilisheheni katika misa ya wafu iliyofanyika katika kanisa katoliki ya Maria Consolata (Cathedral) hapa jimboni Marsabit kwa ajili ya kuombea mwendazake Gabriel Gambare aliyekuwa meneja wa Tume ya Haki na Amani (CJPC) katika shirika la Caritas Marsabit.
Gambare ametajwa kama mtu aliyejijali na kuwasaidia wasiojiweza katika jamii, na alikuwa chombo cha Amani na kuwaunganisha watu katika kaunti ya Marsabit.
Akizungumza kwenye ibada hiyo, baba paroko wa parokia ya Cathedrali hapa Marsabit Padri Tito Makhoha amemsifia Gambare kama mtu mpenda Amani ambaye alikuwa akisaidia jamii ya Marsabit kuishi kwa Amani upendo.
Kwa upande wake naibu gavana wa kaunti ya Marsabit Solomo Gubo amesema kuwa jamii ya Marsabit itazidi kumkumbuka Gambare kama mtu aliyekuwa na bidii katika mambo aliyoyafanya.
Aidha familia imemtaja Gambare kama mtu mchapa kazi ambaye alikuwa akijitolea kuhakikisha kuwa familia yake imeishi kwa furaha wakisema kuwa alikuwa mtulivu na mkarimu ambaye kila mmoja katika familia alikuwa anamtegemea.
Gambare ambaye alizaliwa 1976, alifariki tarehe 08, mwezi novemba 2024 mjini New Delhi, India alipokuwa akipokea matibabu.
Mwenda zake ameacha mke na Watoto sita.
Kabla ya kifo chake, Gambare alikuwa akisomea Shahada ya Uzamili katika chuo kikuu cha African Nazarene jijini Nairobi. Kuanzia 2011 hadi kifo chake, Gabriel alifanya kazi katika shirika la Caritas Marsabit katika nyadhifa mbalimbali.
Pia alihudumu waadhifa wa mwenyekiti wa Teachers Sacco Marsabit na Mwenyekiti wa Shule ya Msingi ya Hulahula ambayo alijitolea sana.