Na Machuki Dennson
Rais William Ruto amewaapisha mawaziri wake 22 hii leo katika ikulu yake ya Nairobi. Zoezi hilo limeongozwa na mkuu wa utumishi wa Umma Felix Kosgei mbele ya rais.
Rais amewaapisha mawaziri hao baada ya mkutano na wajumbe wa mrengo wa Kenya Kwanza katika ikulu hiyo.
Hiyo jana mawaziri hao waliidhinishwa na bunge la kitaifa na muda mfupi baadaye rais akawatangaza rasmi kuwa mawaziri kupitia gazeti rasmi la serikali.
Mawaziri wapya sasa ni kama ifuatavyo:
- Kiongozi wa mawaziri – Musalia Mudavadi
- mwanasheria mkuu – Justin Muturi
- waziri wa maswala ya ndani- Prof Abraham Kindiki
- waziri wa fedha na mipangilio ya kiuchumi – Prof. Njuguna Ndung’u
- waziri wa huduma za kitaifa na maswala ya jinsia – Aisha Jumwa
- waziri wa ulinzi – Aden Duale
- Waziri wa maji na usafi – Alice Wahome
- waziri wa maswala ya kigeni – Alfred Mutua
- waziri wa biashara, uwekezaji na viwanda – Moses Kuria
- waziri wa maswala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, maeneo kame na maendeleo ya ukanda – Rebecca Miano
- waziri wa barabara, uchukuzi na miundomsingi – Kipchumba Murkomen
- waziri wa mazingira na misitu – Soipan Tuya
- waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya miji – Zachariah Mwangi Njeru
- waziri wa utalii, wanyamapori na turathi za kitaifa – Peninah Malonza
- waziri wa kilimo na ufugaji – Mithika Linturi
- waziri wa afya – Susan Nakumicha Wafula
- waziri wa mawasiliano, habari na uchumi wa kidijitali – Eliud Owalo
- waziri wa elimu- Ezekiel Machogu
- waziri wa kawi na petroli – Davis Chirchir
- waziri wa michezo, Sanaa na maswala ya vijana – Ababu Namwamba
- waziri wa mashirika na biashara ndogo ndogo – Simon Chelugui
- waziri wa madini, uchumi wa maziwa kuu na bahari – Salim Mvurya
- waziri wa leba – Florence Bore
- Katibu wa baraza la mawaziri – Mercy Wanjau
Mawaziri hawa watachukua hatamu za uongozi kutoka mawaziri waliohudumu kipindi cha rais mstaafu Uhuru Kenyatta.