Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya Isaac,
Viongozi mbali mbali pamoja na wenyenji wa kaunti ya Garissa wanaendelea kumuomboleza aliyekuwa Seneta wao Yussuf Hajji aliyeaga dunia siku ya Jumatatu.
Maombi Maalum yanatajiwa kuandaliwa katika shule ya Young Muslim kabala ya kuelekea nyumbani kwake Ijarra.
Waziri wa fedha Ukur Yattani, Gavana wa Garissa Ali Korane, Gavana wa Isiolo Mohamed Kuti, Kiongozi wa Mashtaka Nchini Nordin Hajji, Wabunge pamoja na viongozi mbalimbali wa kaunti hiyo wanatajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Hajji aliaga dunia akiwa katika hospitali moja ya Nairobi jumatatu asubuhi alipokuwa akipokea matibabu.
Marehemu Hajji atakumbukwa kwa kuliongoza jopo lililokusanya maoni ya wakenya na kisha kuandaa ripoti ya mwisho ya BBI.
Mwendazake alizikwa mnamo siku ya jumatatu katika Maziara ya Kiislamu ya Lang’ata jijini Nairobi.