Local Bulletins

Tume Ya NCIC Ipewe Nguvu Zaidi – Wasema Waadhiriwa Wa Ghasia Za Baada Ya Uchaguzi Wa Mwaka Wa 2007/2008.

Picha; Hisani

By Waihenya Isaac

Vuguvugu la wakimbimzi wa ndani kwa ndani walioadhirika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007/2008 wamependekeza mageuzi ya sheria ili kuipa tume ya Uiano na Utengamano Nchini NCIC nguvu zaidi.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Kitale waadhiriwa hao wametaja kuwa ni vyema tume ya NCIC imepewa nguvu zaidi ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuzuia kurejelewa kwa machafuko kama yaliyojiri baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007/2008 katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022.

Wametaja kuwa joto la kisiasa ambalo limekuwa likishuhudiwa humu nchini hususan mvutano uliopo katika Ripoti ya maridhiano BBI huenda ukagawanya taifa hili zaidi.

Wadhiriwa hao wametoa changamo kwa  asasi mbali mbali za serekali kuwajibika ili kuhakikisha kuwa wanasiasa pamoja na wananchi hawaenezi semi za chuki.

Aidha wameiahidi kuendeleza kampeni ya kutaka viongozi wachochezi kuchukuliwa hatua na hata kuzuuiwa kuwania  nafasi za uongozi katika chaguzi zijazo.

 

Subscribe to eNewsletter