Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya Isaac
Tume ya Uiano na Utengamano Nchini NCIC imeelezea kusikitishwa kwake na namna mwakilishi wa kike Katika kaunti ya Isiolo Rehema Jaldesa alivyojiwasilisha Katika afisi zao hii leo.
NCIC ilikuwa imemwagiza Rehema Jaldesa kufika mbele ya tume hiyo mida ya saa nne asubuhi kabla ya kupokea barua kutoka kwa wakili wake George Kithi iliyoeleza kuwa mbunge huyo atajiwasilisha baadae saa tisa mchana.
Aidha Mbunge huyo alifika Katika makao ya NCIC akiwa ameandamana na wabunge Qalicha Gufu wa Moyale, Ali Dido Rasso wa Saku, Ali Wario wa Bura, Hassan Odha Hulufo wa Isiolo Kaskazini,pamoja mwakilishi wa kike katika kaunti ya Marsabit Safia Sheikh Adan.
Inaarifiwa kuwa viongozi hao waliagiza kukutana na Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari Samuel Kobia ambaye alikuwa anahudhuria mkutano na badala yake wakatakiwa kuonana na makimishna wawili wa tume hiyo jambo ambalo walisusia na kuondoka.
Rehema Jaldesa alitakiwa kujiwasilisha mbele tume ya NCIC baada ya madai kuwa matamshi yake yalichochea jamii na kusababisha machafuko Katika kaunti za Isiolo na Marsabit.