Raia 9 wa Eritrea na wawili Ethiopia wapigwa faini ya Sh50,000 au kifungo cha miezi 2 kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
February 24, 2025
By Waihenya Isaac,
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Katika shule ya wavulana ya King David Kamama Katika kaunti ya Embu aliyepatikana akiwa na risasi pamoja na mwenzake aliyepatikana akijaribu kutetekeza Bweni wanazuiliwa Katika kituo cha polisi cha Manyatta kaunti ya Embu.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Katika kaunti hiyo Daniel Rukunga kuwa kuwa njama ya kuteketeza Bweni la shule ilitibuliwa na mlinzi wa shule baada ya kuwashuku wanafunzi kadhaa na walipoitwa ili kukaguliwa ndipo mmoja akapatikana na risasi ya milimita 7.6 inayoweza kutumika Katika bunduki kama AK 47.
Wakti uo huo wasichana 24 ambao walikamatwa Katika shule ya upili ya wasichana ya Ndagaiya kauti hiyo ya Embu wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani mjini Runyenjes hii leo.
Wasichana hao pamoja na mfanyikazi mmoja wa shule hiyo wanakabiliwa na mashtaka ya uteketezaji wa shule.